Mtaalamu wa hati za kiarabu kutoka China Ustadh (Nuru-Dini Mi Qawanj Jayanj) ameandika barua ya shukrani kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar baada ya kupewa zawadi, kutokana na kushiriki kwake kwenye maonyesho ya turathi ya kimataifa awamu ya pili, yaliyo simamiwa na idara ya turathi chini ya idara ya habari katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, chini ya anuani isemayo (Tabia tukufu), yaliyo fanywa katika eneo la katikati ya Ataba mbili takatifu kuanzia tarehe (20 – 25 Novemba 2021m).
Muandishi huyo alishiriki akiwa na mabango mawili aliyoandika maandishi ya kiarabu kwa mfumo wa kichina, akaongeza uziri wa maonyesho na kuvutia macho ya watu wengi.
Idara ya Ataba imethamini ushiriki wake, imempongeza na kukubali kazi yake, imempa zawazi ya pesa na cheti cha shukrani, baada ya kupokea zawadi hizo kutoka Atabatu Abbasiyya, akaandika barua ya shukrani, barua hiyo ipo kama ifuatavyo:
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu
Shukwani za pekee ziende kwa Atabatu Abbasiyya tukufu..
Na mheshimiwa katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar..
Kwa kunizawadia baada ya kushiriki kwangu maonyesho ya turathi ya kimataifa awamu ya pili..
Kutoka kwa ndugu yenu bwana Nuru-Dini Mi Qawanj Jayanj kutoka jamhuri ya watu wa China”.
Tambua kua maonyesho yalikua na ushiriki wa kimataifa, miongoni mwa nchi zilizo shiriki ni Misri, Iran, China, pamoja na wenyeji Iraq.