Maahadi ya Qur’ani tukufu inaendelea kufanya vikao vya kielimu katika Maqaam ya Imamu Hujjat (a.f)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea kufanya vikao vya kielimu ndani ya Maqaam ya Imamu Mahadi Almuntadhir (a.f), kwa kushirikiana na uongozi wa Maqaam hiyo tukufu.

Wanahitimu Qur’ani nzima kila baada ya miezi minne, chini ya usimamizi wa Shekh Ali Rawii, katika vikao hivyo husomwa Qur’ani tukufu na kubainisha hukumu za tajwid sambamba na kufafanua sehemu zinazo weza kutumiwa na wapotoshaji na kueleza usahihi wake katika usomaji.

Katika vikao hivyo pia hufundishwa maarifa ya Qur’ani kupitia aya tukufu na hadithi za Ahlulbait (a.s), tambua kuwa vikao hivyo hufanywa baada ya swala ya Magharibi na Ishaa kila siku.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu inaendesha program na miradi tofauti, sambamba na kusimamia vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya vituo vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kufundisha Qur’ani na kuchangia katika kutengeneza jamii yenye uwelewa wa Qur’ani kwenye sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: