Maahadi ya Qur’ani tukufu kwa kushirikiana na idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, inaendesha ratiba ya ufundishaji wa Qur’ani tukufu kwa mazuwaru na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ndani ya haram kwa muda wa jioni baada ya swala ya Ishaa na Magharibi siku nne kwa wiki.
Ratiba hiyo inasimamiwa na kiongozi wa idara ya usomaji wa Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani Ustadh Alaau-Dini Hamudi Alhamiri, kufuatia kauli ya Mtume mtukufu isemayo: (Mbora wenu ni yule atakaejifunza Qur’ani na akaifundisha) na kwa lengo ya kutangaza utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa usahihi, sambamba na kusikiliza kwa makini na kutafakari aya zake na hukumu zake.
Wakati wa usomaji wa Qur’ani hufundishwa hukumu za usomani na fani zake, mbele ya mazuwaru watukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na hutolewa ufafanuzi unaosaidia kuboresha usomaji wao, pamoja na kutaja baadhi ya maana za maneno ya Qur’ani sambamba na kubainisha nyeradi za swala na kurekebisha makosa.