Kupokea wanafunzi 420 wa semina za Qur’ani za wasichana kwa siku moja

Maoni katika picha
Semina za Qur’ani zinazo endeshwa na Maahadi ya Qur’ani kwa wasichana katika mkoa wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, ni jambo kubwa katika utendaji wake na yameandaliwa mazingira mazuri yanayo endana na usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Siku ya Ijumaa hushuhudiwa harakati kubwa zinazo husu Qur’ani, kwani asilimia kubwa ya semina hutolewa katika siku za mapumziko, utawakuta wanafunzi wanamiminika Maahadi kwa ajili ya kushiriki kwenye semina, idadi ya wanafunzi waliopokelewa imefika (420) kutoka makundi tofauti na wenye umri tofauti, ambao watashiriki kwenye semina (32) za aina tofauti, zipo semina za usomaji wa Qur’ani, kuhifadhi na tafsiri.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Katika siku ya Ijumaa Maahadi ilipokea wanafunzi (420) kutoka shule tofauti, wameiahidi Maahadi kuwa watashiriki masomo mwaka mzima na watadumisha mawasiliano, wameonyesha ham kubwa ya kujifunza Qur’ani tukufu, na kuhakikisha jambo hilo haliathiri safari yao ya masomo, hivyo asilimia kubwa wanahudhuria masomo katika siku ya Ijumaa, kwani ndio siku pekee ya mapumziko katika wiki”.

Akafafanua kuwa: “Jumla semina zinafika (32), wanafundishwa usomaji, hukumu na kuhifadhi, wanahudhuria kwa zamu tatu, ratiba yao inaanza saa mbili asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni, hii ni kutokana na idadi ya madarasa ya kufundishia Qur’ani tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: