Shindano la (Duraru-Fatwimiyyah) la wasichana

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza hatua ya kwanza ya shindano la (Duraru-Fatwimiyya) la wasichana, sambamba na kumbukumbu ya kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Shindano linalenga kuibua vipaji vya ushairi kwa wanawake na usomaji wake katika kueleza dhulma aliyofanyiwa mtoto wa Mtume (s.a.w.w), usomaji wa mashairi unaonyesha kiwango cha mapenzi kwa mama huyu mtakatifu.

Masharti ya shindano:

  • - Kuandika kaswida inayo mzungumzia bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ianze na ubeti usemao (Mbavu ilichomwa msumari damu ikatoka ** na dunia yote inalia kwa kudhulumiwa Fatuma).

Kisha ukamilishe beti za kaswida hiyo zitakazo endana na maana ya ubeti wa kwanza.

  • - Kaswida izingatia kanuni za vina na uzani wa mashairi.
  • - Beti za kaswida zisiwe chini ya kumi (10).
  • - Mwisho wa kupokea kaswida hizo ni tarehe 2/12/2021m.
  • - Kaswida zote zitumwe kwenye telegram kwa link ifuatayo @khitabamedia

Kaswida zote zitawasilishwa kwenye jopo la majaji watakao zishindanisha na kupata mshindi mmoja tu, jina lake litatangazwa siku ya kumbukumbu ya kifo cha Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili, mshindi atapewa zawadi ya dinari laki moja na elfu hamsini (150,000), hali kadhalika kaswida zote zilizo timiza masharti ya vina na uzani pamoja na majina ya watunzi wake zitawekwa kwenye mtandao wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: