Kamati ya maelekezo na msaada wa kimaana inaendelea kutembelea vikosi vya wapiganaji wa Hashdu-Sha’abi

Maoni katika picha
Kamati ya maelekezo na msaada wa kimaana chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya imetembelea kikosi cha opresheni ya Ambaar cha Hashdu-Sha’abi, chini ya ratiba yake maalum ya kutembelea vikosi vya jeshi na Hashdu-Sha’abi katika vikosi mbalimbali vilivyopo nchini.

Kiongozi wa kikosi hicho Ahmadi Nasrullah ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Tumepokea ugeni kutoka kamati ya maelekezo ya Dini na msaada wa kimaana chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao umekuja kutembelea kikosi cha opresheni ya Ambaar cha Hashdu-Sha’abi, wametembelea maeneo ya kikosi chetu na kuangalia mambo mbalimbali”.

Akafafanua kuwa: “Ugeni umewasilisha salamu na dua kutoka kwa Marjaa Dini mkuu na katibu Mkuu wa Atabatu Abbasiyya, pamoja na kutoa mawaidha na kueleza usia wa Marjaa Dini mkuu kwa mujahidina, hali kadhalika wametembelea makao makuu ya opresheni na maeneo ya viongozi”.

Wapiganaji wamepongeza juhudi za Atabatu Abbasiyya pamoja na uwepo wake wa kudumu katika uwanja wa vita na kwenye maeneo yaliyokombolewa, wakasisitiza kuwa matukio kama haya yanawatia nguvu ya kuendelea kuwa ngome Madhubuti dhidi ya kila anayetaka kuharibu amani na utulivu wa taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: