Kitengo cha maadhimisho kinajiandaa kufanya kongamano la awamu ya kumi na tano la msimu wa huzuni za Fatwimiyya

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kinajiandaa kufanya awamu ya kumi na tano ya kongamano la msimu wa huzuni za Fatwimiyya.

Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan amesema: “Kongamano litafanywa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya usimamizi wa kitengo chetu”, akaongeza kuwa: “Litadumu kwa muda wa siku kumi, litakua na vipengele tofauti vya uombolezaji, pamoja na kueleza sehemu ya Maisha ya Zaharaa (a.s)”.

Akabainisha kuwa: “Bibi Zaharaa (a.s) anastahiki zaidi ya hayo, tunaadhimisha kumbukumbu ya kifo chake kwa anuani ya Ashura ndogo, vyovyote tutakavyo fanya hatuwezi kutekeleza haki ya Zaharaa (a.s)”.

Akafafanua kuwa: “Kufanya maadhimisho haya ni sehemu ya kuangazia baadhi ya dhulma alizofanyiwa (a.s)”.

Kumbuka kuwa kongamano huandaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kila mwaka kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: