Wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu wanaendelea na masomo yao kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Maoni katika picha
Idara ya Tahfiidh katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, inaendelea na masomo yake ya kila siku kwa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi kitabu kitakatifu.

Wakufunzi ni walimu wenye weledi waliochaguliwa na Maahadi baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na baada ya kuandaa muongozo wa kufundisha vizito viwili vitakatifu, na mbinu tofauti za kuhifadhisha.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu imeandaa sehemu muwafaka ya kusomea, iliyowekwa vifaa vyote vya kusomea.

Tunapenda kukumbusha kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kufundisha elimu ya Qur’ani na kuandaa jamii ya wasomi wa Qur’ani na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: