Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinaendelea kutoa semina na warsha kwa watumishi wapya wa shule za Al-Ameed

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinaendelea kutoa semina kwa walimu waliojiunga na shule za Al-Ameed hivi karibuni.

Kiongozi wa idara ya taaluma Ustadh Amiri Saadi amesema kuwa: “Semina zinahusu mambo muhimu katika sekta ya ufundishaji, mawasiliano na usimamizi pamoja na namna ya kutekeleza mkakati wa Rafiki Zaairu”.

Akaongeza kuwa: “Warsha zinazofanywa kuna za malezi na za elimu, lengo ni kuwaandaa watumishi wapya”, akafafanua kuwa: “Tumefanya warsha katika sekta ya usimamizi wa malezi pamoja na warsha ya Rafiki Zaairu, aidha watapewa semina kuhusu vifaa vya kufundishia siku zijazo”.

Kumbuka kuwa semina na warsha hizi zinalenga kuwajengea uwezo watumishi wa shule za Al-Ameed.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: