Kituo cha utamaduni wa familia kinatoa wito wa kushiriki kwenye semina ya njinsi ya kuamiliana na vijana

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa wito wa kushiriki kwenye semina ya pili yenye anuani isemayo (muongozo wako wa kuamiliana na vijana), semina hii inafanywa baada ya kupatikana mafanikio makubwa katika semina kama hii iliyotangulia.

Mkuu wa kituo bibi Sara Hafaar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Semena hii ni maalum kwa wakina mama tu, watafundishwa kulingana na mazingira halisi ya Maisha pamoja na kupewa mifano hai ya mambo halisi yaliyotokea, tutaonyesha changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua”.

Akaongeza kuwa: “Semina itaanza tarehe nne ya mwezi ujao, miongoni mwa mada zitakazo fundishwa ni: (changamoto za ujana – kuongea na vijana), pamoja na mambo mengine pia tutasikiliza changamoto kutoka kwa washiriki”.

Kumbuka kuwa semina itafanywa kwa njia ya mahudhurio ndani ya ukumbi wa kituo uliopo Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali ya Imamu Hussein (a.s), ndani ya jengo la kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s), usajili wa kushiriki kwenye semina hiyo unafanywa kwa njia ya telegram kupitia link ifuatayo: @Thaqafaasria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: