Maahadi ya Qur’ani tukufu na chuo kikuu cha kimataifa Almustwafa zimefungua ushirikiano

Maoni katika picha
Ugeni kutoka chuo kikuu cha kimataifa cha Almustwafa umetembelea Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kujenga ushirikiano baina yao.

Tumeongea na Shekh Akram Naamani muwakilishi wa chuo hicho hapa Iraq kuhusu ziara yao, amesema: “Tumefurahi kutembelea Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, ziara yetu imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano”, akaongeza kuwa: “Tutashirikiana katika mambo tofauti yanayo husu Qur’ani, kama vile kuendesha semina, nadwa, mashindano, makongamano ya kimataifa na mengineyo ambayo maahadi imeonyesha ipo tayali kushirikiana na sisi”.

Akaendelea kusema: “Ziara hii inaimarisha ushirikiano baina ya pande mbili, na tutaandaa mkataba wa makubaliano kati yetu”, akasema: “Tunapongeza kazi nzuri inayofanywa na Maahadi katika sekta ya Qur’ani na juhudi za watumishi wake wanaofanya kazi kwa weledi ndani na nje ya Iraq, kwa lengo la kufundisha masomo ya Qur’ani na mafundisho ya Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani ni moja ya vituo vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kufundisha elimu ya Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwezo wa kufanya tafiti katika sekta zote za Qur’ani tukufu na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: