Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imefungua semina mpya tano

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefungua semina mpya tano.

Semina hizo zinahusu kufundisha usomaji wa Qur’ani kwa njia rahisi kwa wanafunzi wanao anza pamoja na kuwafundisha hukumu za usomaji na kuhifadhi, wanafunzi wamewekwa kwa makundi kulingana na viwango vyao na umri wao.

Maahadi inawakufunzi mahiri wenye uwezo mkubwa wa kufundisha Qur’ani tukufu.

Semina hizo ni: “Semina ya Jua, semina ya Swafaat na semina ya Muzammil), aidha kuna (Semina ya Zaharaa) ya kuhifadhi Qur’ani tukufu, na (Semina ya Rahmaan) itaendeshwa kwa njia ya mtandao kwa wale ambao watashindwa kuja darasani”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake hufanya semina za Qur’ani kipindi chote cha mwaka, sambamba na kutoa mitihani kila wakati kwa wanafunzi wake kwa lengo la kuandaa kizazi cha wasichana wasomi wa Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: