Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya upasuaji nadra kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka (25) aliyekua na tatizo la kubana mirija ya uzazi, wamesisitiza kuwa vifaa-tiba vya ospitali na weledi wa madaktari na wauguzi ndio sababu kubwa ya mafanikio hayo.
Daktari bingwa wa upasuaji wa sikio, pua, na mirija ya uzazi Dokta Naadhim Amrani amesema: “Jopo la madaktari limefanikiwa kuzibua mirija ya uzazi kwa daraja la tatu, kwa kutumia teknolojia ya Leza iliyopo katika hospitali ya rufaa Alkafeel, sambamba na kutumia vifaa-tiba vya kisasa katika upasuaji.
Akasisitiza kuwa: “Upasuaji huo umefanikiwa kutokana na umahiri wa jopo la madaktari na wasaidizi wao” akasema: “Baada ya upasuaji hali ya mgonjwa iliimarika na akaruhusiwa kutoka hospitali”.
Daktari wa upasuaji amesema: “Upasiaji ulihitaji maandalizi ya vifaa-kazi na maandalizi hayo yalifanywa kwa ukamilifu”.
Tambua kua hospitali ya rufaa Alkafeel hutoa huduma za kisasa daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa na madaktari mahiri kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa duniani.
Kumbuka kuwa Hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali mbalimbali za maradhi yao.