Idara ya umeme chini ya kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya imemaliza kupamba jengo la amalalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuweka taa kila sehemu, kazi hiyo ni sehemu ya kukamilisha kazi zote za ujenzi katika jengo hilo tukufu, baada ya kumaliza miradi yote mikubwa ya ujenzi sasa tunakamilisha uwekaji wa mapambo.
Kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wetu wanaofanya kazi ndani ya hara tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanamajukumu mawili makubwa, kwanza ni kukarabati sehemu zote za jengo na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, na jukumu la pili ni kuboresha na kuweka taa za mapambo”.
Akaongeza kuwa: “Taa za mapambo zimewekwa juu ya kila paa la haram, kwa namna ya kiislamu na mwanga mzuri, unao ongeza uzuri wa muonekano”.
Akabainisha kuwa: “Taa hizo zimefungwa kwenye ghorofa la juu na sehemu ya tabaka la chini, kila tabaka lina taa (57)”.
Kumbuka kuwa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa vitengo muhimu, kina idara nyingi, mafundi na mainjinia wa kitengo hicho wanafanya kazi usiku na mchana katika maeneo tofauti ya Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kutoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu.