Usomaji wa Qur’ani wa pamoja umeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Hindiyya

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya, limeratibu usomaji wa Qur’ani kwa pamoja kupitia semina nne za Qur’ani.

Ratiba hii inalenga kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa usahihi na kufuata hukumu za usomaji, kusimama na kuanza, thawabu za kisomo hicho zimeelekezwa kwa mashahidi wa Iraq.

Kiongozi wa tawi la Maahadi katika mji wa Hindiyya Sayyid Haamid Mar’abi amewataka wanafunzi waendelee kushikamana na vizito viweli vitakatifu kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume.

Akasema kuwa tawi linaharakati nyingi katika maeneo tofauti zinazo lenga kufundisha Qur’ani kupitia semina na nadwa.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu cha kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya na inalenga kusambaza elimu ya Qur’ani, na kutengeneza jamii ya wasomi wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika mambo tofauti ya Qur’ani na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: