Kazi ya kutengeneza dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) inaendelea, siku baada ya siku watumishi wanasonga mbele katika utendaji wao, wa kuendelea kukamilisha sehemu zilizo baki, sehemu ya mwisho ni kuweka vipande vinavyo tengenezwa kwenye umbo la mbao, lililopo ndani ya ukumbi wa kiwanda cha kutengeneza madirisha ya makaburi matukufu na milango mitakatifu chini ya Atabatu Abbasiyya.
Miongoni mwa vipande vilivyo kamilika hivi karibuni, ni vipande vya maandishi ya mashairi ambavyo maandishi yake yamezungushiwa ufito wa dhahabu, utakao wekwa baadae sehemu ya juu ya dirisha, ambayo ni moja ya sehemu za maandishi, dirisha hili linamaandishi ya Qur’ani ambayo yamesha kamilika, na maandishi ya shairi ambayo yanatenganishwa na pambo liitwalo (Alkalwa).
Rais wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitakatifu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Naadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maandishi ya mashairi yanavipande (28) vinazunguka dirisha pande zote nne, kuna vipande viwili juu ya kila chumba cha dirisha, vimeandikwa kaswida ya mshairi la Ali Swafaar Alkarbalai yenye anuani isemayo: (Ni Zainabu), imeanza kwa kusema:
Ni Zainabu mtoto wa uongofu .. Babari ya ukarimu na utukufu.
Mtoto wa Mtume mtakatifu .. Roho yangu najitolea kwa wake utukufu.
Beti hizo ndio kibwagizo cha hiyo kaswida hadi mwisho, maandishi ya kaswida hiyo yameandikwa na mtaalamu wa hati za kiarabu Dokta Raudhwani Bahiyya kwa hati ya Thuluth”.
Akaendelea kusema: “Kila kipande cha maandishi ya shairi kina ukubwa wa (mlm5) na kimo cha (sm16) na urefu wa (sm30), maandishi ni ya dhahabu halisi na kitako cha maandishi ni cha madini ya mina ya kijani”.
Akamaliza kwa kusema: “Maandishi yamekaa vizuri, nayo ni katika mapambo yaliyo ongezwa katika kazi hii, yametengenezwa kwa ustadi na weledi wa hali ya juu, yanaonekana kuma kitu kimoja”.
Kumbuka kuwa kazi ya kutengeneza dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) inaenda kama ilivyo pangwa, kila sehemu ya utendaji wake imefanywa kama ilivyo kusudiwa, sawa iwe sehemu ya madini au mbao, kila sehemu inayo kamilika inaunganishwa kwenye umbo la mbao, ambalo ndio kazi ya kwanza hufanywa katika utengenezaji wa dirisha.