Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimepokea wageni kutoka chuo kikuu cha Bagdad, na kimeandaa ratiba maalum yenye vipengele vingi.
Kupokea ugeni wa wanafunzi ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, na program ya kongamano la kitamaduni la kila wiki linalo lenga kudumisha mawasiliano na vijana, ambao ni kundi muhimu katika jamii, kwani wao ndio mustakbali na nguzo ya Iraq.
Mkuu wa utekelezaji wa ratiba Ustadh Hussein Shaakir Atwaar kutoka idara ya mahusiano ya vyuo na shule katika kitengo tajwa, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Siku ya Ijumaa tumepokea wanafunzi zaidi ya (50) kutoka chuo kikuu cha Bagdad, ratiba ya mapokezi yao ilifunguliwa na ibada ya ziara na kusoma dua kwa pamoja ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya hapo walikaribishwa na kutambulishwa harakati zinazofanywa na idara hii kwa ujumla, na mradi uitwao (kijana mzalendo wa Alkafeel)”.
Akaongeza kuwa: “Katika ratiba hiyo umetolewa mhadhara kuhusu maendeleo ya taifa na Ustadh Jasam Saidi kutoka kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya, chini ya anuani isemayo: (Kuimarisha utambulisho wa taifa na namna ya kuulinda), ameongea kuhusu utambulisho wa taifa na uzalendo, akafahamisha maana ya kuwajibika na haki za raia na wajibu wake, na vipi anaweza kujiandaa kwa ajili ya kutumikia taifa katika sekta zote, akasisitiza kuwa kunahaja kubwa ya kulea nafsi na kuzifundisha uzalendo”.
Akaendelea kusema: “Baada ya hapo wakatembelea korido za haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na makumbusho ya Alkafeel, ambapo wameangalia mali-kale za thamani na vifaa adimu vya kihistoria”.
Akaongeza kuwa: “Baada ya hapo ugeni ukaelekea katika haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa ajili ya kufanya ziara, halafu wakaenda kutembelea mji wa Sayyid Auswiyaa (a.s) chini ya Atabatu Husseiniyya (a.s), na hapo ndio kikawa kituo cha mwisho”.
Ugeni umeshukuru watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kazi kubwa na tukufu wanayo fanya ya kumtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake watukufu.