Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Baabil na chuo kikuu cha Qassim wanajadili njia za kushirikiana

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya, umetembelea chuo kikuu cha Qassim katika mji wa Baabil kwa ajili ya kujadili ushirikiano wa pande mbili.

Rais wa chuo kikuu cha Qassim Dokta Hassan Awadi ameonyesha utayali wa chuo hicho kushirikiana na Maahadi, akasisitiza kuwa milango ya Chuo iko wazi kwa Ataba tukufu kwa maslahi ya Qur’ani hapa nchini.

Naye kiongozi wa tawi la Maahadi akaeleza miradi itakayo fanywa mwaka huu, miongoni mwa miradi hiyo ni nadwa za kielimu, semina za Qur’ani, mashindano ya kuandika pamoja na harakati tofauti katika vyuo na Maahadi zilizopo katika mkoani Baabil.

Tambua kua tawi la Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Baabil hufanya harakati tofauti za Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kusambaza elimu ya Qur’ani na kutengeneza jamii yenye uwelewa wa Qur’ani tukufu
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: