Makamo kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Semina hii inatokana na jinsi Atabatu Abbasiyya inavyo ona umuhimu wa kuweka mazingira mazuri, Ataba imekunjua mikono na kuwashika wasichana katika kuendeleza vipaji vyao kwenye sekta ya elimu, utamaduni na michezo, kwa kutumia ratiba rafiki kwa makundi yote”.
Akaongeza kuwa: “Semina inafanywa siku moja kwa wiki, kwa kiasi ambacho haiharibu ratiba ya masomo ya washiriki, itadumu kwa muda wa mwaka mzima, chini ya wakufunzi mahiri na wenye uzowefu mkubwa kwa makundi yote, miongoni mwa mambo watakayo fundishwa ni:
- - Masomo ya mihadhara hukusu mbinu za uwasilishaji.
- - Masomo kuhusu mbinu za kutoa khutuba.
- - Masomo kuhusu Maqamaat za Qur’ani.
- - Masomo ya Fiqhi na Aqida.
- - Masomo kuhusu uimbaji.
- - Kuna mambo mengi, kama kusoma upigaji wa picha, uandishi, uchoraji na kazi za mikono”.
Akabainisha kuwa: “Washiriki wa semina wanatoka katika mkoa wa Karbala, Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua jukumu la kuwasafilisha kutoka majumbani mwao hadi katika ofisi za idara, kwenye kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) cha harakati za wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Kumbuka kuwa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imefungua semina hii kutokana na kuongezeka kwa idadi ya washiriki na matokeo mazuri ya semina zilizo tangulia.