Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kukarabati kituo cha afya cha Adliy katika mji wa Karbala

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kukarabati kituo cha afya cha Adliy katika mkoa wa Karbala, kazi hiyo ni sehemu ya harakati ya ujenzi katika mkoa wa Karbala, kwa lengo la kusaidia idara ya afya katika mkoa huu, na kuingiza katika orodha ya mafanikio.

Msimamizi wa kazi hii Ustadh Hassan Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi wa kitengo, watumishi wa idara ya mitambo na vifaa pamoja na shughuli za ujenzi, wameanza kukarabati sehemu hiyo, kwani ilikua imeanza kuharibika”.

Akaongeza kuwa: “Tumeanza kwa kubaini sehemu zinazo hitaji matengenezo, kisha tukaanza na kazi ya kuondoa marumaru za zamani za chini na ukutani, na kusawazisha sakafu kwa vifaa maalum, hii ni hatua muhimu ya kazi kwani ndio msingi wa kazi zingine”.

Akabainisha kuwa ukarabati huo utahusisha:

  • - Kuweka marumaru sakafu na ukuta.
  • - Kuweka mfumo mpya wa umeme.
  • - Kutengeneza mfumo wa kusambaza maji.
  • - Kuweka mfumo wa maji taka.
  • - Kukarabati njia na milango.
  • - Kutengeneza milango na madirisha.
  • - Kuongeza eneo la bustani.

Pamoja na kazi zingine zitakazo fanywa kama zilivyo pangwa.

Kumbuka kuwa kazi ya kukarabati ni sehemu ya miradi ya kibinaadamu inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya mkakati wa ukarabati wa majengo ya serikali kwa ajili ya kudumisha huduma zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: