Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya ukarabati wa madawati katika shule za mkoani Karbala kwa kushirikiana na idara ya malezi na idara za shule, kwa lengo la kuchangia sekta ya elimu hapa mkoani na kuweka mazingira mazuri ya kusoma kwa wanafunzi.
Rais wa kitengo cha ujenzi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Mhandisi Samiri Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, watumishi wa kitengo chetu wameanza kazi ya kukarabati madawati mabovu mashuleni, hasa kwenye shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi”.
Akaongeza kuwa: “Kazi hiyo ni muendelezo wa kazi zingine zilizo tangulia katika shule hizo, ikiwa ni pamoja na kuboresha taasisi za shule”.
Akabainisha: “Hatua za kwanza wameshiriki mafundi selemala na mafundi chuma, nayo ilikua ni kazi ya kubaini mahitaji, kisha ikafuata kazi ya matengenezo, awamu ya kwanza tumetengeneza zaidi ya madawati (150)”.
Mkuu wa shule za Karbala ameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa msaada huu na kuwaomba waendelee kutoa misaada kwa maslahi ya wanafunzi.
Kumbuka kuwa kazi ya kukarabati madawati ni sehemu ya mradi wa huduma za kibinaadamu unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kukarabati baadhi ya majengo ya serikali yaliyochakaa, hasa majengo ya shule, hospitali na taasisi zinazotoa huduma za kijamii.