Chuo kikuu Al-Ameed kimesaini mkataba wa ushirikiano wa kielimu na chuo kikuu cha Bagdad

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kimesaini makubaliano ya ushirikiano na chuo kikuu cha Bagdad kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu na tafiti katika vyuo hivyo.

Mkataba uliosainiwa na rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Muayyad Ghazali na rais wa chuo kikuu cha Bagdad Dokta Muniri Saadi una vipengele vingi ikiwa ni pamoja na kufanya nadwa, makongamano, semina na warsha za kielimu kwa pamoja.

Mkata huo pia umeeleza ufanyaji wa semina za kujenga uwezo kwa watumishi wa vyuo hivyo, na kufanya miradi ya utafiti ya pamoja, sambamba na kubadilishana uwezo na uzowefu kupitia ratiba zitakazo shirikisha walimu na wanafunzi wa vyuo hivyo.

Aidha mkataba huo umehusisha ushirikiano wa ofisi za vyuo viwili katika mambo yote, bila kusahau mambo yanayohusu wanafunzi, na kuboresha ratiba ya elimu na maabara pamoja na mambo ya mitandao.

Mkataba huo umetoa nafasi ya kutumia maabara za vyuo vyote viwili katika kufundisha na kufanya tafiti, baada ya kuwasiliana vitivo husika.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya kila kiwezalo katika kuboresha huduma zake kwenye sekta ya elimu, utamaduni, malezi na tafiti za kielimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: