Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram kwa kushirikiana na idara ya ushonaji katika kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya, wameweka mabango na vitambaa vyenye ujumbe wa pongezi, korido za Ataba tukufu zimepambwa vizuri kwa ajili ya kusherehekea tukio hilo takatifu, aidha maua yamewekwa katika haram tukufu ya Abulafadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuwashwa taa za rangi na kufukiza marashi.
Miongoni mwa mambo yatakayo fanywa katika maadhimisho hayo ni:
- - Kufanya hafla kubwa itakayo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni.
- - Program ya wiki ya Zainabiyya kwa wasichana itakayo simamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake.
- - Kufanya halfa za wanawake chini ya idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wakike.
- - Kutoa mihadhara ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kitaandaa vipindi maalum kuhusu maadhimisho hayo.
- - Kufungua milango ya kujiandikisha kufanyiwa ziara kwa niaba katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) kupitia ukurasa maalum uliopo katika mtandao wa Alkafeel.
- - Kuweka masayyid wahudumu ndani ya ukumbi wa haram tukufu kwa ajili ya kugawa pipi na maua kwa mazuwaru.