Kuzaliwa kwa heshima na fahari ya waja wema Hauraa Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Mama mtakatifu Fatuma Zaharaa (a.s) katika siku kama ya leo mwezi tano Jamadal-Uula, alimzaa bibi Zainabu (a.s), hajawahi kuzaliwa mtu kama yeye katika uislamu, kwa jinsi alivyo kuwa na Imani, utukufu, heshima na jihadi.

Watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na maswahaba walipokea tukio hilo kwa furaha kubwa, kiongozi wa kiislamu akafanya kanuni za kisheria, akamsomea adhana katika sikio la kulia na kumsomea iqama kwenye sikio la kushoto, hivyo sauti ya kwanza aliyosikia ilikua ni (Allahu Akbaru, Laa ilaaha illa Llah), nayo ndio maneno yaliyokua yakisemwa na mitume na msingi wa kuumbwa ulimwengu.

Maneno hayo yalikaa katika moyo wa Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), yakawa ni sehemu ya uwepo wake, akakulia katika nyumba yenye watu watatu watukufu zaidi kushinda viumbe wote wa Mwenyezi Mungu, nao ni (Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ali kiongozi wa waumini na Fatuma mbora wa wanawake wa duniani (a.s).

Zaharaa (a.s) akampa mtoto Imamu (a.s), akamchukua na kuanza kumbusu, Zaharaa akamuambia “mpe jina”, Imamu akamjibu: “Siwezi kumtangulia Mtume (s.a.w.w)..”. Imamu (a.s) akamuambia Mtume (s.a.w.w) ampe jina, Mtume akasema: “Siwezi kumtangulia Mola wangu…”. Akaja Jibrilu (a.s) kutoka mbinguni akamuambia Mtume (s.a.w.w) “Mtoto huyu mpe jina la Zainapu (a.s) hakika Mwenyezi Mungu amemchagulia jina hilo”. Kisha akamuambia mitihani atakayo pata mjukuu wake huyo, Mtume na watu wa nyumbani kwake wakaanza kulia.

Bibi Zainabu (a.s) alilelewa katika nyumba ya elimu na maarifa, nyumba ya wahyi, aliishi kati ya shule ya Utume na Uimamu, akahitimu shule zote mbili, aliishi chini ya uangalizi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na wasii wake Ali bun Abutwalib (a.s), na mama wa baba yake Fatuma Zaharaa (a.s) Mbora wa wanawake wa duniani, na Hassan na Hussein (a.s) mabwana wa vijana wa peponi, hakika anafaa kuwa kigezo cha wanawake wema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: