Ataba mbili tukufu zinatoa pole kwa familia za mashahidi na watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea mkoa wa basra

Maoni katika picha
Ugeni kutoka ataba mbili tukufu umewasili katika mkoa wa basra kutoa pole kwa familia za mashahidi na watu walio jeruhiwa kwenye shambulizi la kigaidi lililotokea hivi karibuni katika hospitali ya mkoa na kusababisha vifo vya watu wanne na idadi kubwa ya majeruhi.

Rais wa ugeni huo kutoka Atabatu Abbasiyya sheikh Aadil Wakiil ameuaambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumeunda ugeni kutoka Ataba mbili tukufu chini ya maelekezo ya viongozi wakuu wa kisheria ili kuja kuwapa pole familia zilizopoteza wapenzi wao katika shambulio la kigaidi lililofanya na maadui wa ubinaadamu. Tunatoa pole kwa famila za mashahidi na tunamuomba Mwenyezi Mungu hawaweke mahala pema peponi mashahidi wetu, na awape subira na uvumilivu wafiwa, na awaponye haraka majeruhi, tumeahahidi kutoa ushirikiano katika kuwatafuta na kuwabaini magaidi hao na kuhakikisha wanafikishwa kwenye mikono ya sheria”.

Akaongeza kuwa: “Familia za mashaidi na majeruhi wamepewa zawadi kutoka katika malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.f), pamoja na kuwaombea maghafira mashahidi na kuwatakia kupona haraka majeruhi”.

Tambua kuwa ugeni umehusisha viongozi wakubwa kutoka Ataba mbili tukufu, wamewasilisha rambirambi za marjaa Dini mkuu na viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba hizo na watumishi, famila za mashahidi, sambamba na kuwaombea majeruhi wapone haraka.

Famila za mashahidi na majeruhi wameshukuru sana kutembelewa na ujumbe huo, na wamewapa pole ya uchovu wa safari, aidha wamefurahishwa na hatua zilizo chukuliwa na ataba mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: