Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inawapa semina walimu wa malezi ya kiislamu, jumla ya walimu (25) wanashiriki kwenye semina hiyo.
Semina inafanywa kwa kushirikiana na idara ya malezi ya wilaya ya Hindiyya, wamefundishwa masomo yanayo husu hukumu za usomaji, mbinu za ufundishaji, matamshi ya herufi na sifa zake, pamoja na somo la Fiqhi na Aqida, chini ya walimu waliobobea katika masomo hayo.
Semina imefanywa kwa muda wa siku mbili, nayo ni sehemu ya harakati za Qur’ani zinazo fanywa na tawi katika shule za Hindiyya, kwa lengo la kufundisha vizito viwili vitakatifu.
Semina hii inalenga kuongeza uwezo wa walimu na kuwafanya waelewe hukumu za usomaji wa Qur’ani na fani zake.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani kupitia matawi yake tofauti, ni kituo muhimu cha kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kufundisha elimu za Qur’ani na kujenga jamii yenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu kuhusu sekta zote za Qur’ani tukufu na fani zake.