Kituo cha turathi za Basra kinafanya nadwa ya turathi kuhusu historia ya mji wa Barsha

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kinafanya nadwa yenye anuani isemayo (Kuzaliwa kwa Basra ya Othmaniyyuun/ historia kwa ujumla).

Nadwa imefanywa ndani ya ofisi za kituo chini ya uhadhiri wa mwalimu wa kitivo cha malezi na elimu za kibinaadamu -kutoka chuo kikuu cha Basra- Dokta Shukuri Naswiri Abdulhassan na Dokta Hussein Ali Ubaidi, wameongea kwa undani kuhusu ukweli wa Othmaniyya walio tawala kwa muda unaokaribia karne nne.

Nadwa imepambwa na maoni kutoka kwa washiriki pamoja na maswali, ambapo watoa mada wamejibu na kufafanua kwa kina baadhi ya mambo.

Nadwa inalenga kuangazia wakati muhimu kihistoria katika mji wa Basra.

Tambua kuwa kituo cha turathi za Basra, ni kituo kinacho jihusisha na kuhuisha turathi pamoja na kuzitangaza, kina machapisho mengi yanayo zungumzia turathi, na kimesha fanya nadwa nyingi na maonyesho mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: