Kuanza ukarabati na uwekaji wa vioo kwenye kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi na ujenzi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kazi ya kukarabati na kuweka vioo kwenye kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, baada ya kumaliza ukarabati wa ukuta na paa la haram tukufu.

Rais wa kitengo tajwa Mhandisi Samiri Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kazi hii ni sehemu ya jukumu la ukarabati wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) linalo tekelezwa kwa kufuata ratiba iliyowekwa sambamba na kuheshimu utukufu wa kubba, na kuzingatia athari za usanifu wa kihandisi”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya ukarabati inayofanywa na idara ya maraya katika kitengo chetu, imehitimishwa kwa kuweka vipande vya maraya katika haram tukufu na kuta zake, na kuhamia sehemu muhimu ambayo ni sawa na moyo wa kazi hiyo, nayo ni sehemu ya kubba tukufu, kazi inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Kuondoa marumaru za zamani na viyoo pamoja na vitu vingine vilivyo kuwa vimebandikwa ukutani.
  • - Kukarabati mfumo wa umeme, taa na kamera.
  • - Kukarabati ukuta kwa kutumia vifaa maalumu kulingana na mahitaji ya kila sehemu.
  • - Kubadilisha viyoyozi na kuweka vya kisasa.
  • - Kufanya usanifu maalumu wa nakshi, vioo na ujenzi wa vipande vya maraya kwa kufuata vipimo maalumu”.

Akabainisha: “Vifaa vitakavyo tumika katika kazi hii vimesha andaliwa, ni vifaa imara, vya kisasa, vyepesi na Madhubuti, sambamba na kuzingatia usanifu wa zamani na kuhakikisha baada ya kumaliza kazi hii panakua na muonekano mzuri unao endana na sehemu zingine za haram”.

Kumbuka kuwa kazi zote zinafanywa kwa ustadi na weledi mkubwa chini ya utendaji wa wahandisi wa kiiraq miongoni mwa watumishi wa kitengo, kazi inaendelea vizuri bila kikwazo chochote au kutatiza harakati za mazuwaru, na kwa kuzingatia mpango kazi uliowekwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: