Ugeni kutoka idara ya malezi ya mkoa wa Misaan ulio husisha wakuu wa shule za mkoa huo, umetembelea shule za Al-Ameed katika mji wa Karbala.
Ugeni huo umetembelea maeneo ya shule na kuangalia ubora wa majengo na usanifu wa kisasa katika ujenzi wa shule ndani ya jamii, wameangalia ukubwa wa madarasa, vifaa vya kufundishia pamoja na maeneo ya wazi na viwanja vya michezo vya kisasa.
Mwisho wa matembezi yao, ugeni umesifu maendeleo waliyo shuhudia katika mfumo wa malezi na elimu, wakapongeza kazi inayofanywa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ya kuandaa kizazi chenye kujitambua cha watu wenye elimu na maarifa.
Tambua kuwa shule za Al-Ameed ni sehemu ya taasisi ya kielimu yenye program mbalimbali za kielimu, sambamba na program za kuwajengea uwezo watumishi wake ili kuwafanya waendane na maendeleo ya dunia, sambamba na kuwawezesha kuhudumia jamii katika nyanja tofauti za Maisha.