Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Baabil na idara ya malezi ya mkoa zimeazimia kufanya miradi kadhaa ya Qur’ani

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, umetembelea idara kuu ya malezi katika mkoa wa Baabil, kwa ajili ya kujenga ushirikiano wa kufanya miradi ya Qur’ani hapa mkoani.

Katika ziara hiyo miradi kadhaa inayoweza kufanywa kwa ushirikiano imejadiliwa, miongoni mwa miradi hiyo ni semina za Qur’ani kwa wanafunzi wa malezi ya kiislamu na walimu, na mradi wa swala bora kwa wanafunzi.

Aidha wamejadili kuhusu mashindano ya Qur’ani kwa wanafunzi wa shule za hapa mkoani, sambamba na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wenye sauti nzuri, kupitia semina za kuwajengea uwezo, na mambo mengine ya kukuza vipaji.

Idara imeonyesha utayali wake kupitia mazungumzo yaliyofanywa na mkuu wake pamoja na wageni hao, amepongeza uwezo mkubwa walionao Ataba katika kusambaza elimu ya Qur’ani kwa wanafunzi na walimu, akasisitiza kuwa taasisi ya malezi ikotayali kufanya harakati yeyote kwa kushirikiana na Ataba tukufu.

Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati tofauti zinazo husu Qur’ani, pamoja na kuendesha semina endelevu za Qur’ani hapa mkoani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: