Kituo cha kuelekeza wanafunzi waliosajiliwa katika chuo kikuu cha Alkafeel kinaendelea kutoa huduma kwa wanafunzi

Maoni katika picha
Kituo cha kuelekeza wanafunzi waliosajiliwa katika chuo kikuu cha Alkafeel, kinaendelea kutoa huduma zake kwa wanafunzi wanaopenda kujisajili kwenye vyuo vikuu binafsi.

Kazi hiyo inafanywa siku zote za kazi katika wiki, ispokua siku ya Ijumaa, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, kwenye ofisi zake zilizopo chuo kikuu cha Alkafeel/ jengo la udaktari wa meno/ mjini Najafu.

Kumbuka kuwa kituo hiki kilifunguliwa kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kufanya maombi ya kujiunga na chuo kwa njia ya mtandao, chini ya maelekezo yaliyotolewa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Kituo kina kamati zifuatazo: (kamati ya mapokezi, kamati ya usajili kwa njia ya kawaida, kamati ya usajili kwa njia ya mtandao, kamati ya uhakiki).

Kwa maelezo zaidi fika katika ofisi za chuo zilizopo Najafu/ barabara ya (Najafu – Karbala) mkabala na nguzo namba 23/ mtaa wa Nidaa/ Jirani na nyumba za makazi Amiraat, au tembelea toghuti yake https://alkafeel.edu.iq au piga simu kupitia moja ya namba zifuatazo:

  • Ofisi ya mkuu wa chuo: 07601839901 na 07803880900.
  • Kitengo cha usajili na mambo ya wanafunzi: 07601393393.
  • Kitengo cha mali: 07601888183.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: