Maahadi ya Qur’ani tukufu inaanza mradi wa semina za Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Baabil

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imeanza mradi wa semina za Qur’ani katika vyuo vikuu vya Baabil.

Mkuu wa tawi la Maahadi katika mkoa wa Baabil Ustadh Muntadhiri Mashaikhi amesema: “Chuo kikuu cha kiislamu kimekua cha kwanza, wanafunzi wa masomo ya Qur’ani na lugha wamefundishwa mada mbalimbali za Qur’ani, chini ya walimu bobozi”.

Akaongeza kuwa: “Mosomo haya yanatokana na makubaliano ya awali kati ya chuo kikuu na Maahadi, chuo kinawajibika na masomo ya nadhariyya na Maahadi mada za usomaji”. Akabainisha kuwa: “Tumeshuhudia muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi wanaoshiriki kwenye semina hii na wakufunzi pia”.

Semina hizi zinalenga kuimarisha usomaji wa Qur’ani, na mafundisho ya vizito viwili.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu, imetembelea vyuo vikuu na Maahadi na kuweka utaratibu wa kufundisha Qur’ani katika vyuo hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: