Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu umeshuhudia ufunguzi wa kongamano la huzuni za Fatwimiyya awamu ya kumi na tano, ambalo hufanywa kila mwaka na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili, baada ya watumishi wa kitenge cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kumaliza kazi ya maandalizi, chini ya kamati ya maandalizi ya kongamano, kama sehemu ya ufunguzi rasmi utakao fanyika Alasiri ya siku ya Ijumaa.
Kongamano hilo ni sehemu ya kuwatukuza watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na kuomboleza kifo cha mtoto wa Mtume (s.a.w.w) bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ambaye siku ya kifo chake ilikua mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar kwa mujibu wa riwaya ya pili.
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kongamano hili linafanywa kwa mwaka wa kumi na tano, nalo ni miongoni mwa makongamano muhimu yanayo fanywa na kitengo chetu kila mwaka, katika kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) na kubainisha dhulma alizo fanyiwa, kongamano hili limepewa jina la Ashura ndogo”.
Akaongeza kuwa: “Kongamano litakua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni maonyesho ya sauti na picha, mambo muhimu kutoka katika Maisha ya Zaharaa (a.s), kutakua na ushiriki wa baadhi ya maktaba za Karbala kwa kuweka machapisho yao mbele ya wanakongamano na mazuwaru, sambamba na makundi mbalimbali ya watu wa Karbala kushiriki kwenye shughuli maalum za uombolezaji, kutakua na mambo mengine mengi yatakayo fanyika katika siku za kongamano”.
Kumbuka kuwa tangu miaka kumi na nne iliyopita, uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu umekua ukiomboleza kifo cha bibi Fatuma (a.s) kwa muda wa siku kumi na kuziita (Muharam ndogo), kwa kufanya kongamano lenye vipengele mbalimbali vinavyo endana na anuani ya kongamano (kongamano la huzuni za Fatwimiyya).