Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kongamano la shahada ikiwa na shehena kubwa ya vitambu mbalimbali

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, imeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu yanayofanywa kwenye kongamano la shahada la kumi na moja, chini ya kauli mbiu isemayo: (kumtambua bibi Fatuma Zaharaa -a.s- ni njia ya kuokoka kwa umma), yanayo simamiwa na taasisi ya kitamaduni ya Imamu Hussein (a.s) na idara ya mawakibu Husseiniyya katika mtaa wa Dabuni mkoani Waasit, na kushirikiana na Ataba tukudu za (Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya, Abbasiyya), pamoja na uongozi wa chuo kikuu cha Waasit.

Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake katika kila maonyesho, limeshiriki likiwa na shehena kubwa ya vitabu vya aina tofauti vinavyo endana na malengo ya maonyesho, na lengo la maonyesho haya ni kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Tawi hili limekuja na vitabu vya aina tofauti vyenye lengo moja, vimejaa mafundisho ya Dini – Utamaduni – Elimu – Sekula – Turathi – Maendeleo – Historia, pamoja na majarida yanayohusu watoto na wanawake na mengineyo, aina zaidi ya (250) ya vitabu vilivyo shiriki, vitabu hivyo vimevutia watu wengi ikiwemo kamati ya maandalizi ya kongamano, bila kusahau kulikua na kitabu maalum kinacho muhusu bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Msimamizi wa kongamano hili Shekh Haazim Abudi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kila awamu ya kongamano hili, Atabatu Abbasiyya tukufu huwa na mchango maalum, jambo hili limesha zoweleka, tawi la Ataba linavitabu vinavyo lenga makundi yote, tunatarajia mtu anayekuja kwenye maonyesho haya afaidike kielimu na kitamaduni”.

Kumbuka kuwa kongamano husaidiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kushiriki kwake kwenye mambo tofauti, huchangia katika utoaji wa mihadhara, hufanya warsha na nadwa mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: