Ugeni kutoka kitivo cha kilimo katika chuo kikuu cha Karbala, uliojumuisha walimu na wanafunzi, umesema kuwa miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kilimo, inatekelezwa kwa kutumia elimu ya kisasa, na imekua na mafanikio makubwa, hayo ndiyo tuliyosikia kutoka kwa wasimamizi.
Ugeni ukaendelea kusema kupitia mjumbe wao Dokta Khalid Abdumatwar “Hakika ni kitu kizuri sana kupata mtu anayebadilisha jangwa kuwa kijani kibishi na mahala pazuri kwa kilimo kwa kutegemea uwezo wa raia wa Iraq”.
Wameyasema hayo katika ziara iliyoratibiwa na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ugeni huo umetembelea shamba la kunazi na mashamba ya khairaatu Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na shirika la Khairul-Juud la teknolojia ya kilimo cha kisasa, wamesikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa kila mradi, miongoni mwa teknolojia za kisasa zinazo tumika na kuleta mafanikio makubwa kwenye sekta ya kilimo ni aina ya mbolea inayo tumika.
Mwisho wa ziara, ugeni umeshukuru Ataba tukufu kwa kuwapa nafasi ya kuja kuangalia miradi ya Ataba, ukizingatia kuwa nafasi ya pekee kwa wanafunzi wa kilimo kuangalia vifaa na teknolojia inayotumika kwenye kilimo cha kisasa, wakasema kuwa wanatarajia ziara za aina hii ziendelee siku zijazo.