Katikati ya haram mbili ya mwanae na ndugu yake: Kufunguliwa kwa kongamano la kumi na tano la huzuni za Fatwimiyya

Maoni katika picha
Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu Alasiri ya leo siku ya Alkhamisi (11 Jamadal-Uula 1443h) sawa na tarehe (16 Desemba 2021m), limefunguliwa kongamano la huzuni za Fatwimiyya awamu ya kumi na tano, chini ya usimamizi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Ufunguzi wa kongamano hilo umehudhuriwa na viongozi wa Ataba mbili tukufu, pamoja na wawakilishi wa mawakibu za Karbala na kundi kubwa la mazuwaru.

Ufunguzi wa kongamano ulitanguliwa na mashairi ya kuomboleza yaliyosomwa na Shekh Muhsin Asadi na Karaari Hussein Karbalai, aidha kulikua na ujumbe kutoka kwa rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan, ameongea kuhusu ukubwa wa tukio hili na umuhimu wa kongamano la kuhuisha kifo cha bibi Zaharaa (a.s), akafafanua kuwa: “Kongamano litadumu kwa muda wa siku kumi, kutakua na vipengele vya uombolezaji vitakavyo husu kueleza Maisha ya bibi Zaharaa (a.s)”, akabainisha kuwa: “Zamani kongamano hili lilikua linafanywa siku moja tu, hakika bibi Zaharaa (a.s) anastahiki zaidi ya hivyo, tumefanya kumbukumbu ya kifo chake huombolezwa kwa muda wa siku kumi na kuziita Ashura ndogo”.

Wasimamizi wa kongamano wametembelea maonyesho hayo, wakiwa na rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan, ambaye amefafanua kila kipengele kwenye maonyesho hayo.

Tambua kuwa maonyesho haya hufanywa kila mwaka kama sehemu ya kukumbuka msiba mkubwa uliotokea katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w), msiba wa kufiwa na mtoto wake na burudisho la jicho lake mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili, huwa kuna vipengele vingi vya uombolezaji sambamba na kueleza historia ya bibi mtakatifu anaye kumbukwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: