Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Maqam ya Imamu Mahadi (a.f) katika mji wa Karbala, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s), chini ya usimamizi wa Baabu-Salaamah kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, majlisi zitafanyika kwa siku tatu, waimbaji mbalimbali wanashiriki, pamoja na kuhudhuria kundi kubwa la waombolezaji na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo cha Maqaam bwana Adnaan Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ratiba ya uombolezaji iliyoandaliwa na Atabatu Abbasiyya katika kukumbuka kifo cha mtoto wa Mtume (s.a.w.w) bibi Zaharaa (a.s), inavipengele vingi, kuna mambo yanayo fanywa na Ataba yenyewe kupitia vitengo vyake moja kwa moja na mambo ambayo haifanyi moja kwa moja bali inashiriki kwenye utekelezaji, zikiwemo majlisi hizi, ambazo zimeandaliwa na kikundi kongwe hapa Karbala kikundi cha Baabu-Salaamah”.

Akaongeza kuwa: “Majlisi inafanywa kwa muda wa siku tatu, jioni baada ya swala ya Ishaa kwenye moja ya kumbi za Maqaam, hufunguliwa kwa Qur’ani tukufu ambayo husomwa na bwana Baasim Karbalai, hufuatiwa na muhadhara kutoka kwa Shekh Hussein Khaqaani, huzungumza mambo tofauti, hueleza historia tukufu ya bibi Zaharaa (a.s), kisha hufanywa majlisi ya matam ambayo hushiriki muimbaji Samiri Waailiy na Ali Yusufu na kuhitimishwa na muimbaji Mula Baasim Karbalai”.

Akabainisha kuwa: “Watumishi wa Maqaam wametoa huduma nzuri kwa washiriki, sambamba na huduma zinazo tolewa na baadhi ya vitengo na idara za Atabatu Abbasiyya, kama kitengo cha habari, kitengo cha vipaza sauti na kitengo cha ushonaji”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum kwa ajili ya maombolezo haya, yenye vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kufanya mihadhara ya kuomboleza ndani na nje ya mji wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: