Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imeratibu semina ya kielimu kwa wanafunzi wa Dini

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya, imeratibu semina inayohusu kuandika tafiti ya kielimu, chini ya mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini.

Wanasemina wanafundishwa namna ya kufanya tafiti za kielimu kwa kufuata misingi ya uandishi, itawasaidia kujiepusha na makosa katika uandishi wa tafiti za kielimu, na kuwafanya kuwa bora kielimu na kimaarifa.

Wanasemina wanakaribia wanafunzi (30) kutoka kwenye hauza ya Najafu.

Wanafunzi watakao fanya vizuri watapewa zawadi kwenye hafla ya kufunga semina na vyeti vya ushiriki, huku mshindi wa kwanza akipewa zawadi maalum.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake yote ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, kinacholenga kufundisha masomo ya Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa na maarifa ya Qur’ani kwenye sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: