Maukibu ya maombolezo ya Husseini (a.s) ya Ataba mbili tukufu inafanya maombolezo baada ya kusimama kwa miaka miwili

Maoni katika picha
Maukibu ya maombolezo ya Imamu Hussein (a.s) ya watumishi wa Ataba mbili tukufu Huseiniyya na Abbasiyya, imeanza harakati za uombolezaji baada ya kusimama kwa zaidi ya miaka miwili kwa sababu ya janga la Korona na kutii maelekezo yaliyo tolewa na wizara ya afya, leo wamerudi tena kuanza uombolezaji wa pamoja katika kumbukumbu ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Kama kawaida matembezi ya kuomboleza yameanza baada ya Adhuhuri ya Jumamosi (13 Jamadal-Uula 1443h) sawa na tarehe: (18 Desemba 2021m), chini ya utaratibu wa mikusanyiko na matembezi uliowekwa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wamesimama kwa mistari na kutoa pole kwake kutokana na msiba huu, baada ya hapo walianza kutembea wakiongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqari na wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, halafu wakaenda kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, huku wakiimba kaswida na tenzi za kuomboleza, mazuwaru wa malalo mbili takatifu pia waliungana nao kwenye matembezi hayo.

Maukibu ilipokaribia kuingia katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) ilipokewa na watumishi wa malalo hiyo na kuungana pamoja nao, wakafanya kwa pamoja ibada ya ziara halafu wakafanya majlisi ya matam na kaswida zinazo muhusu mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mambo yaliyo mtokea kabla ya kifo chake hadi kufikia kifo chake, hakika alidhulumiwa na akafa akiwa kavunjika mbazi yake.

Kumbuka kuwa maukibu ya Ataba mbili tukufu ilianzishwa (17 Muharam 1427h) chini ya maelekezo ya makatibu wakuu wa Ataba mbili tukufu, maukibu hiyo imeendelea kuwepo hadi leo, imekua ikiomboleza tukio hili kila mwaka sambamba na kufanya maadhimisho mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: