Matembezi ya wanawake ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s) mbele ya malalo ya mwanae na ndugu yake (a.s)

Maoni katika picha
Malalo mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), jioni ya jana siku ya Jumamosi (13 Jamadal-Uula 1443h), zimeshuhudia kuwasiri kwa maukibu ya wanawake ya kuomboleza, kawaida kila mwaka hufanya maombolezo haya kwa mujibu wa riwaya ya pili, maombolezo haya yapo katika ratiba ya msimu wa huzuni za Fatwimiyya za kumi na tano, chini ya usimamizi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Kwenye matembezi hayo wameshiriki watu wengi wenye majina ya Fatuma kwa ajili ya kuomboleza msiba wa wajina wao, wakina mama hao walitanguliwa na Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu waliokuwa wamebeba jeneza la kuigiza kama ishara ya jeneza la mtoto wa Mtume (s.a.w.w), pamoja na kundi la watoto waliojaa huzuni wakiwa wamebeba mishumaa, baada ya kusimama kwa mistari walianza kutembea kwenda katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanya maombolezo ya kwanza.

Kisha wakaelekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu wakipita katikati ya makundi ya mazuwaru, huku wanaimba qaswida za kuomboleza hadi wakaingia katika haram ya mfiwa Abu Abdillahi Hussein (a.s), na kumpa pole ya kufiwa na mama yake Fatuma Zaharaa (a.s).

Kumbuka kuwa hakukuwa na mawakibu za wanaume peke yake, bali kulikua na mawakibu za waombolezaji wanawake pia, baada ya kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu kuweka mazingira rafiki kwa wote, kuanzia mwanzo wa matembezi hadi mwisho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: