(Mimi nasoma) toleo jipya la kituo cha tafiti za kielimu

Maoni katika picha
Hivi karibuni katika kituo cha tafiti za kielimu chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimetoa kitabu miongoni mwa tunzi za mtafiti Hussein Manati chenye jina lisemalo (Mimi nasoma).

Kitabu hiki ni miongoni mwa machapisho ya kituo yanayo husu utamaduni na muongozo, muandishi ameeleza mambo yanayohusu uwezo wa mwanaadamu katika kupambana na mitihani ambayo huwa kikwazo kati yake na matumaini yake.

Ameandika maudhui za kitamaduni na kimaendeleo, yanayo husu vijana katika swala hilo tukufu, kwa mfano: (Usidanganye nafsi yako, hisia zako ni muhimu, wafanye wakae kimya, hisia za nguvu na salama, eleza maoni yako, kubali ukweli wa kifo, jiamini) na maudhui zingine nyingi zinazo jenga ushujaa kwa vijana.

Tambua kuwa kituo cha utafiti wa kielimu kinafanya kazi mwaka mzima ya kutafiti na kuandika vitabu vinavyo lenga kujenga uwezo wa kijana wa kiislamu, sambamba na kuingiza vitabu vipya kwenye maktaba.

Ukihitaji kupata nakala yako ya kitabu fika kwenye maonyesho ya vitabu ya kudumu katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: