Ugeni wa Atabatu Abbasiyya umempongeza katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya kwa kupewa cheo hicho

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu wametembelea malalo ya kiongozi wa waumini (a.s).

Baada ya kufanya ziara na kusoma dua chini ya kubba la malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) walienda katika ukumbi wa wageni wa Atabatu Alawiyya, kumpongeza katibu mkuu mpya Sayyid Issa Khurasani kwa kupewa kwake madaraka hayo, naye aliongoza mapokezi akiwa na wajumbe wa kamati yake.

Ugeni umefikisha salamu na pongezi za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na kumuombea mafanikio katika kazi yake ya kutumikia malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) na mazuwaru wake.

Mkutano umeshuhudia kubadilishana maneno matam ya ukaribisho na kujadili njia za ushirikiano na mawasiliano baina ya Ataba mbili tukufu Alawiyya na Abbasiyya, na kila jambo linalohusu kuhudumia mazuwaru na miradi inayohusu shughuli hizo.

Mkutano ukahitimishwa kwa kukabidhi zawadi ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa Sayyid Khurasani na zawadi zingine, na kumuomba Mwenyezi Mungu ampe nguvu za kutekeleza jukumu lake, naye Sayyid Khurasani aliwaombea kukubaliwa ziara yao na ibada walizo fanya na kurudi salama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: