Program (katika kila nyumba muokozi) inaendelea na semina zake

Maoni katika picha
Wataalamu wa Alkafeel wa masomo ya uokozi na matibabu chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu wanaendelea na semina za program ya (katika kila nyumba muokozi) kwa watumishi wa kitengo cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkufunzi bwana Ahmadi Yahya Mussawi amesema: “Lengo la semina hizi ni kuandaa watu watakao weza kutoa huduma ya uokozi ya haraka, katika kuhudumia mazuwaru na jamii kwa ujumla”.

Akaongeza kuwa: “Semina mbili zimefanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Imamu Swadiq (a.s), semina moja imefanywa asubuhi na nyingine jioni, kila semina imetumia saa sita za masomo, walengwa wa semina hizo ni wahudumu wa vitengo vinavyo hudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) moja kwa moja”.

Akaendelea kusema: “Semina imekua na mada tofauti, miongoni mwa mada hizo ni, mbinu za kuokoa mtu mwenye tatizo la moyo, uokozi wa watoto na wazee, kujikinga na magonjwa ambukizi”.

Naye mkufunzi Muhammad Bayati akasisitiza kuwa: “Ni muhimu kueneza utamaduni wa elimu ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza katika jamii”. Akasema: “Jamii inatakiwa kujua mbinu za kupambana na majanga na namna ya kuokoa waathirika kielimu”.

Tambua kuwa programu inamasomo ya nadhariya na vitendo, kuna jumla ya wakufunzi kumi na moja, ili kurahisisha kufundisha kwa njia ya vitendo na kutoa kazi ya mbinu walizo fundisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: