Idara ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuanza kwa shindano la marafiki wa Mwenyezi Mungu la kusoma surat Alhamdu kwa watoto wenye umri wa miaka (4 – 8) wa jinsia zote mbili.
Watashiriki kwa kutuma video za ushiriki, wasome kwa ufasaha pamoja na kutaja jina la msomaji, umri na mkoa, kisha atutumie kwenye telegram kwa anuani ifuatayo: @Alwahda_alqurania.
Video zote za ushiriki zitakabidhiwa kwenye kamati ya majaji watakao zichuja na kupata washindi.
Video zinapokelewa kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe 1 Januari 2022 hadi tarehe tatu, washindi wanapewa zawadi.
Shindano hili linatokana na jinsi idara ya Qur’ani inavyo jali kundi hili sawa na makundi mengine yaliyo fanya mashindano siku za nyuma, sambamba na umuhimu wa kuhifadhi sura hiyo tukufu, kwani lazima sura hiyo isomwe katika swala za faradhi za kila siku.