Wanafunzi wa mradi wa Haqibatul-Qur’aniyyah wameanza kufanya mitihani katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Wanafunzi wa Maahadi tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kufanya mitihani chini ya mradi wa Haqibatul-Qur’aniyyah hatua ya kwanza na pili.

Mitihani inahusu masomo ya hukumu za usomaji, tajwidi, lugha ya kiarabu, mantiki, fiqhi, historia ya Qur’ani, misingi ya tafsiri, kusimama na kuanza.

Wanafanya mitihani ya aina mbili, nadhariyya na vitengo, itafanyika kwa muda wa wiki mbili mfululizo, baada ya kusoma miezi sita (6), watakao faulu watafundishwa masomo ya ngazi nyingine.

Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Baabil linafanya harakati nyingi zinazohusu Qur’ani sambamba na semina endelevu za Qur’ani tukufu.

Tunapenda kusema kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya vituo vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya yenye lengo la kusambaza elimu ya Qur’ani, na kuchangia katika kuandaa jamii yenye uwelewa wa mambo ya Qur’ani tukufu na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: