Balozi wa Ujerumani nchini Iraq ametembelea Atabatu Abbasiyya na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria

Maoni katika picha
Barozi wa Ujerumani nchini Iraq Mheshimiwa Martin Yighi ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu leo siku ya Jumatano (17 Jamadal-Uula 1443h) sawa na tarehe (22 Desemba 2021m), na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar.

Katika kikao chao wamejadili mambo mengi, Sayyid Swafi amemkaribisha mgeni wake na kumpongeza kwa kupewa madaraka hayo, na akamtakia mafanikio mema katika kutekeleza jukumu ya ubalozi katika jiji la Bagdadi, aidha akasifu kazi zinazofanywa na Ujerumani pamoja na mashirika yake hapa Iraq, na viwanda vyake ambavyo vinaaminika sana na raia wa Iraq.

Kisha akataja baadhi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo imepata mchango mkubwa kutoka kwa mashirika ya Ujerumani, kama vile miradi ya uchapishaji, viwanda, afya na makumbusho, mwisho wa kikao hicho balozi amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta tofauti.

Barozi ameonyesha kufurahishwa kwake kutokana na ziara hii, kwani ndio ziara yake ya kwanza katika mkoa wa Karbala, akasema: “Nimekuja kuutambua zaidi mji huu na Ataba zake takatifu, ziara imekua nzuri na nimefanikiwa kujua mambo mengi, nimekutana na viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, nimesikiliza miradi wanayo fanya na ushirikiano uliopo kati yake na mashirika ya Ujerumani, nitajitahidi kuimarisha ushirikiano huo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: