Kongamano la kitamaduni la wanawake linatoa wito wa kushiriki kwenye shindano la kitafiti

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni la wanawake mwaka wa nne, linalo ratibiwa na maktaba ya Ummulbanina (a.s) ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa wito kwa watafiti wa kushiriki kwenye shindano la kitafiti litakalo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Kukuza ubunifu wa kifikra na kitamaduni ni wajibu wetu).

Mada zitakazo shindaniwa ni:

  • - Athari za matumizi ya elektronik katika huduma za maktaba baada ya janga la Korona.
  • - Miradi mikubwa ya maktaba ya kuendeleza maktaba za umma.
  • - Mchango wa maktaba katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
  • - Maktaba za watoto baina ya upatikanaji na uwepo.

Kanuni za tafiti:

  • 1- Utafiti uambatanishwe na wasifu wa muandishi, uwe haujawahi kutolewa mahala polote na utakabidhiwa kwenye kamati ya majaji.
  • 2- Utafiti unatakiwa kuwa na maneno (300) na uandikwe kwa lugha ya kiarabu.
  • 3- Utafiti uandikwe kwa hati ya Arial na ukubwa wa saizi (12).
  • 4- Kuwe na ukurasa wa vitabu rejea utakao andikwa kwa hati ya Arial na ukubwa wa saizi (12).
  • 5- Siku ya mwisho ya kupokea fupisho za tafiti ni (30/12/2021m).
  • 6- Siku ya mwisho ya kupokea nakala kamili za tafiti ni tarehe 31/01/2022m.
  • 7- Tafiti zitumwe kwa barua pepe ya idara ifuatayo: readingandreceivingunit@gmail.com
  • 8- Tafiti zitakazo shinda wahusika watapewa zawadi.
  • 9- Tafiti zitakazo shinda zitaandikwa kwenye chapisho la kielekronik kwa kushirikiana na jumuiyya ya kielimu Al-Ameed.
  • 10- Washiriki wote watapewa vyeti vya ushiriki.

Kwa maelezo zaidi piga simu kwa namba ifuatayo: (009647602363311) pia namba hiyo inapatikana kwenye whatsapp na telegram.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: