Uombolezaji wa mawakibu za Karbala na pembezoni mwake wakati wa msimu wa huzuni za Fatwimiyya

Maoni katika picha
Mawakibu za Karbala na pembezoni mwake zimeshiriki kwa wingi kwenye maombolezo ya msimu wa huzuni za Fatwimiyya, chini ya usimamizi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, awamu ya kumi na tano ya kuomboleza kifo cha mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Ushiriki ulikua na aina nyingi katika kuhuisha maomboleza hayo kwenye mji wa Karbala makao makuu ya maadhimisho ya Husseiniyya, kulikua na majlisi za kuongea mitihani aliyopitia bibi Zaharaa (a.s) na namna alivyokuwa na subira hadi akaumiza nafsi yake kwa ajili ya kulinda Dini ya baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Majlisi hizo zimepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru wa malalo mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), walisimama kusikiliza yaliyo mtokea mpenzi wao bibi Zaharaa (a.s) katika siku kama hizi mwaka wa 11 Hijiyyah, na watu wa nyumba ya Mtume kwa ujumla (a.s) baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: