Hafla ya siku ya kimataifa ya lugha la kiarabu imefanywa ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Jumuiyya ya kielimu na kifikra Al-Ameed imeadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya kiarabu (lugha ya dhwadi), kwa kufanya nadwa ya kielimu ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya asubuhi ya leo siku ya Ijumaa (19 Jamadal-Uula 1443h) sawa na tarehe (24 Desemba 2021m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Lugha ya vizito viwili: ni msingi wa turathi za kilugha na kifikra duniani), hafla imefanywa kwa kupitia jukwaa la (zoom), wasomi wakubwa wa lugha wameshiriki pamoja na viongozi wa Dini kutoka ndani na nje ya Iraq.

Nadwa imefunguliwa kwa Qur’ani, iliyofuatiwa na usomaji wa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha tukasikiliza wimbo wa taifa na wimbo wa (Lahnul-Ibaa).

Baada ya hapo ukafuata ujumbe kutoka jumuiyya ya Al-Ameed ulio wasilishwa na Dokta Abbasi Fahaam, akaongea kuhusu umuhimu wa lugha ya kiarabu na mchango wake katika historia, kwenye nyanja tofauti za elimu, hakika kiarabu kinamchango mkubwa, akasema kuwa ni lugha ya Qur’ani iliyosifiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu katika aya tofauti, tunamshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametujaalia kuwa miongoni mwa watu wanao ongea kwa lugha ya Qur’ani na wafuasi wa kiumbe bora ambaye ni Mtume Muhammad (s.a.w.w), na akamfanya Imamu wetu kuwa kiongozi wa waumini (a.s), Imamu wa ufasaha na bwana wa waongeaji, tunapongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa hatua hii ya kutaja uzuri wa lugha ya kiarabu na kuhimiza vijana washikamane nayo, kiarabu ni lugha ya Qur’ani na lugha ya Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Kisha mshairi Dokta Hazim Rashki Tamimi na Dokta Ahmadi Jaasim Khiyali wakaimba kaswida zenye beti za kusifu lugha ya kiarabu na umuhimu wa hafla hii.

Ratiba ikaendelea kwa uwasilishaji wa mada za kitafiti chini ya usimamizi wa Dokta Hussein Naswihi, ambapo jumla ya mada tatu ziliwasilishwa kutoka kwa:

  • - Dokta Aadil Abbasi Nasrawi, mada yake ilikua inasema: Lugha ya kiarabu na lugha zingine uhusiano wake na mfanano.
  • - Dokta Majidi Twarish Rabii, mada yake ilikua inasema: Lugha ya kiarabu katika hadithi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s).
  • - Dokta Muhammad Abdushakuur, mada yake ilikua inasema: Lugha ya kiarabu katika mtazamo wa mustashriqina.

Baada ya hapo Dokta Ali Maslawi akawasilisha mkataba wa kurekebisha lugha ya kiarabu hapa Iraq, mwisho wa nadwa watoa mada wakapewa zawadi.

Kumbuka kuwa jumuiya ya kielimu Al-Ameed imesajiliwa rasmi na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu kwa mujibu wa kanuni na sheria ya wizara namba B T – 7199 ya 24/07/2019m, jumuiya hiyo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: