Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kinafanya kongamano la mwaka

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya mkutano wa mwisho wa mwaka pamoja na viongozi na wawakilishi wa ofisi zake za mikoani, jioni ya siku ya Ijumaa (19 Jamadal-Uula 1443h) sawa na tarehe (24 Desemba 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkutano huo umehudhuriwa na wawakilishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na idara ya ulinzi na usalama pamoja na idara ya afya ya mkoa mtukufu wa Karbala.

Rais wa kitengo cha maadhimisho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumezowea kukutana na wawakilishi wetu wa mikoani kila mwaka na kujadili maendeleo na changamoto zinazoweza kutokea katika kufanya maadhimisho ya Husseiniyya wakati wa msimu wa huzuni, hasa kwenye ziara ya Arubaini”.

Akaongeza: “Katika kikao hicho tumewasikiliza wawakilishi wa Ataba mbili, ambao wametoa maoni muhimu na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wawakilishi wetu wa maeneo tofauti, tumejadili na kupata maamuzi ya pamoja, nayo ni kuimarisha kila kitu chenye uhusiano na Imamu Hussein (a.s) na maadhimisho yake”.

Akaendelea kusema: “Kulikua na maoni, maswali na majibu kutoka kwa wawakilishi wa Ataba mbili tukufu kutokana na kilicho wasilishwa kwenye mkutano huo, yataandikwa yote watakayo kubaliana kwa ajili ya kupitishwa kwenye mkutano ujao kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akafafanua kuwa: “Wahudhuriaji wameonyesha umuhimu wa kudumisha maadhimisho na harakati tofauti za Husseiniyya”.

Akahitimisha kwa kusema: “Hali kadhalika kulikua na mazungumzo maalum kati ya viongozi na wawakilishi wa kitengo cha maadhimisho na viongozi wa idara za mji wa Karbala, kwa ajili ya kutatua changamoto zilizo jitokeza kwenye misimu ya ziara zilizopita, idara za kutoa huduma na ulinzi katika mkoa wa Karbala zimeahidi kuongeza juhudi katika kuhudumia mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), na kurahisisha utendaji wa mawakibu ndani ya mipaka ya mkoa wa mtukufu wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: